Rais Barack Obama wa Marekani anatarajiwa kufanya ziara nchini Israel, Ukingo wa Magharibi na Jordan wiki ijayo, miaka mitano baada ya kuyatembelea maeneo hayo matatu akiwa kama seneta. Anatarajiwa kuanza ziara yake hiyo siku ya Jumatano na kuikamilisha nchini Jordan siku ya Jumamosi. Maafisa wa Ikulu ya Marekani wamejaribu kuweka matarajio katika kiwango cha wastani kuhusu kufikiwa kwa hatua yoyote muhimu wakati wa mazungumzo na viongozi wa Israel na Palestina. Obama hatawasilisha mpango mpya wa amani, na pia hatafanya mkutano wa pande tatu, ambao pande hizo zinauhitaji. Naibu mshauri mkuu katika masuala ya usalama wa taifa kwa ajili ya mawasiliano ya kimkakati, Ben Rhodes, amewaambia waandishi habari kuwa ziara hiyo ni kuhusu mazungumzo mapana ya kimkakati na serikali mpya ya Israel. Rhodes amesema kuwa Rais Obama pia analenga katika kuelezea kuunga mkono kwake serikali ya Palestina kuwa ni uongozi halali wa mamlaka hiyo ya Palestina.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO