Sunday, March 17, 2013

WATU WATANO NCHINI INDIA WAKIRI KUMBAKA MTALII

Wanaume watano wamekiri kumbaka mwanamke mmoja  raia wa Uswizi aliyekuwa akitalii kijiji kimoja nchini India wakiwa na mumewe. Kulingana na polisi nchini humo watu hao watano wamekubali walihusika katika ubakaji huo na bado wanawasaka washukiwa zaidi.Mwanamke huyo walikuwa na mumewe wamepiga kambi na  katika msitu mmoja usiku wa Ijumaa walipokuwa wakilizuru eneo hilo la kati kati ya India kwa kutumia baiskeli.Walishambuliwa na genge la kiasi ya wanaume saba ambao walimfunga mumewe kwa kamba na kumbaka mwanamke huyo wa umri wa miaka 39 pamoja na kuwaibia mali zao. Polisi wanawashikilia wanaume 20 kufikia sasa.Kulingana na takwimu kutoka afisi ya kitaifa ya matukio ya uhalifu,kila baada ya dakika 22,mwanamke hubakwa  nchini  India huku makundi ya kutoa misaada yakisema visa vingi huwa haviripotiwi. Kisa hiki cha hivi karibuni kabisa kinawadia miezi mitatu baada mwanamke kubakwa na genge la wanaume ndani ya basi mjini New Delhi na kufariki wakati akitibiwa nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO