Sunday, March 17, 2013

WAASI WA M23 WAWAFUKUZA WAFUASI WA NTAGANDA


Waasi wa Harakati ya M23 wamewafukuza wapiganaji watiifu kwa Jenerali Bosco Ntaganda na kudhibiti tena maeneo yote ya kundi hilo mashariki mwa Kongo. Duru za Umoja wa Mataifa na kundi la M23 jana ziliripoti kuwa, maelfu ya wafuasi wa M23 wamekimbilia nchini Rwanda na wengine kujisalimisha kwa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo baada ya kushindwa na waasi wa M23. Mapigano kati ya makundi hayo mawili yalianza Februari 28 baada ya kiongozi wa kijeshi wa M23 Sultani Makenga kujitenga na  kiongozi wa kisiasa wa kundi hilo  Jean-Marie Runiga na kuanza kushirikina na Ntaganda.
Ntaganda anayejulikana kutokana na vitendo vyake vya kikatili anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC tangu mwaka 2006 akikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya raia.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO