Polisi wa Ujerumani leo wameyavamia maeneo yanayohusishwa na makundi ya waumini wa madhehebu ya Salafi katika majimbo ya kaskazini ya North-Rhine Westphalia na Hesse. Waziri wa Mambo ya Ndani, Hans-Peter Friedrich, ameliambia shirika la habari la Ujerumani, DPA, kuwa mamia ya polisi wamefanya operesheni hiyo kuyasaka makundi ya itikadi kali za kiislamu. Mwaka jana polisi ilifanya msako mkubwa dhidi ya makundi ya Salafi katika majimbo saba ya Ujerumani ya Bavaria, Hesse, North-Rhine Westphalia, Lower Saxony, Hamburg, Schleswig-Holstein na Berlin. Kundi la Kisalafi la Millatu Ibrahim lililokuwa na makao yake katika mji wa Solingen, magharibi ya Ujerumani, lilipigwa marufuku baada ya uvamizi huo. Msemaji wa waziri Friedrich amesema nyaraka zilizonaswa wakati wa operesheni ya mwaka jana, zilitoa habari muhimu zilizotumiwa katika operesheni ya leo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO