Saudi Arabia leo imewanyonga watu saba waliohukumiwa kwa ujambazi, licha ya wito kutoka kwa makundi ya haki za binadamu duniani kutaka wasamehewe. Mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo ameliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu, kuwa watu hao wamenyongwa mapema leo katika uwanja wa Abha, akiongeza kuwa waliuawa kwa kupigwa risasi na wala siyo kuchinjwa kama ilivyo desturi katika nchi hiyo ya kifalme. Tangazo hilo limekuja muda mfupi baada ya Shirika la Kimataifa la Amnesty International kutoa taarifa ikiitolea tena wito serikali ya Saudi Arabia kusitisha mauwaji hayo. Watu hao saba walishtakiwa kwa kupanga kundi la uhalifu, wizi wa kimabavu na kupora katika maduka ya vito vya thamani mnamo mwaka wa 2005, na wakahukumiwa kifo mwaka wa 2009. Wakati wanatenda kosa hilo, bado walikuwa chini ya umri wa miaka 18. Katika mwaka wa 2012 pekee, Saudi Arabia iliwanyonga zaidi ya watu 70.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO