Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Guido Westerwelle ameonya kwamba kuwapatia silaha waasi nchini Syria kunaweza kusababisha kile alichokiita mashindano ya silaha katika eneo hilo na kusisitiza kwamba Umoja wa Ulaya utatuma tu vifaa vya kujilinda.
Katika mahojiano na gazeti la kila siku Tagesspiegel, Westerwelle alisema hali ya mambo nchini Syria ni yakushtusha na kwamba Ujerumani itafanya kila linalowezekana kuchangia katika kupatikana suluhisho la kisiasa, licha ya matatizo yote yalipo.
Lakini akatahadharisha juu ya kuwapa silaha waasi wanaojaribu kumuangusha Rais Bashar al-Assad, baada ya mkuu wa jeshi la waasi la ukombozi wa Syria kusema kwamba wataweza kuuangusha utawala wa Assad katika muda wa mwezi mmoja tu, pindi wakipatiwa silaha zinazofaa. Waziri Westerwelle amesisitiza kwamba Ujerumani na Umoja wa Ulaya zinapaswa kusaidia mapambamno ya waasi hao, lakini haimaanishi tu katika masuala ya kijeshi, bali pia ujenzi wa miundo mbinu na huduma za afya.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO