Saturday, March 09, 2013

UHURU KENYATTA RAIS MPYA WA KENYA HUKU WAPINZANI WAKIJIANDAA KWENDA MAHAKAMANI KUPINGA


Uhuru Kenyata anaonekana kushinda katika uchaguzi mkuu wa Kenya. Matokeo yaliyotolewa leo na tume ya uchaguzi yanaonesha Kenyatta amepata zaidi ya asilimia 50 ya kura zote. Kama ushindi huo ukithibitishwa, atakuwa mshindi wa moja kwa moja na kwamba hakutakuwepo na duru ya pili  ya kupiga kura. Hata hivyo haijwawa wazi kama mpinzani wake anaemfuata kwa karibu, Raila Odinga, ambae ampeata asilimia 43 atayakubali matokeo hayo. Kenyatta ambae ni mtoto wa muasisi wa taifa hilo, ni mtu mwenye utata. Anakabiliwa na mashitaka katika mahakama ya uhalifu ya mjini The Hague, kutokana na madai ya kuhusika katika vurugu za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Baada ya uchaguzi huo zaidi ya watu 1,000 walipoteza maisha katika vurugu zilizodumu kwa miezi miwili, baada Odinga kudai Mwai Kibaki rais wa sasa aliiba kura.
Kwa upande mwingine Muungano wa CORD wake Raila Odinga umeelezea kuwa unajianda kwenda mahakamani kupinga matokeo ya urais yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta. Raila Odinga, ameambia waandishi wa habari kuwa kuwa matokeo yaliyotolewa na tume hiyo yalikuwa yamehujumiwa hasa baada ya kutokea hitilafu katika mitambo ya elektroniki iliyokuwa inatumiwa katika shughuli hiyo. Raila amedokeza kuwa muungano wao unajiandaa kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.

Aidha alisema kugoma kwa mitambo hiyo kulichanganya mambo katika shughuli ya kuhesabu kura. Alisema kuwa baada ya kutokea hitilafu, kura alizokuwa amepata katika maeneo bunge ambayo ni ngome zake , ziliongezwa kwa hesabu ya kura za muungano pinzani wa Jubilee. Mapema wiki hii, wakati shughuli ya kuhesabu kura za urais ilikuwa inafanyika, CORD walielezea malalamishi kuhusu shughuli nzima hasa baada ya kura kuanza kuhesabiwa kwa mikono badala ya mashine. Lakini mahakama kuu ilitupilia mbali kesi yao ikisema kuwa haina uwezo wa kufanya uamuzi katika kesi hiyo, na kuwa ni mahakama ya juu zaidi pakee inayoweza kusikiliza kesi hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO