Sunday, March 17, 2013

UJERUMANI NAYO YAZUIA MATANGAZO YA IRAN


Serikali ya Ujerumani imechukua hatua isiyo ya kawaida ya kuzuia kuonekana nchini humo tovuti ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB. Kwa mujibu wa mwandishi wa IRIB, kuanzia Ijumaa usiku,  Ujuerumani ilichuja na kuzia kuonekana katika intaneti tovuti za zaidi idhaa zaidi ya 30 za kimataifa za IRIB.
Kati ya tovuti za idhaa za IRIB ambazo zimezuiwa Ujerumani ni za idhaa za Kiingereza, Kijerumani, Kiarabu, Kiurdu, Kituruki, Kitaliano na Kifaransa. Hatua ya kukata tovuti ya idhaa za IRIB nchini Ujerumani inakuja baada ya Umoja wa Ulaya EU kukata kanali kadhaa za televisheni na idhaa za za IRIB katika satalaiti. Hatua hizo zimechukuliwa na nchi za Ulaya kwa ushirikiano na Wazayuni kwa lengo la kuzima sauti ya vyombo huru vya habari.
Hivi karibuni Mohammad Sarafraz Mkuu wa kitengo cha kimataifa cha IRIB alisema nchi za Magharibi zinakabiliana na vyombo vya kupasha habari vya Iran mithili ya sheria za msituni.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO