Tume ya uchaguzi ya Venezuela imetangaza kuwa uchaguzi wa rais wa nchi hiyo utafanyika tarehe 14 mwezi ujao wa Aprili. Tangazo hilo limetolewa ikiwa ni siku moja baada ya Nicolas Maduru anayetarajiwa kuchukua nafasi ya Chavez, kuapishwa kuwa rais wa muda wa nchi hiyo katika hafla zilizosusiwa na mrengo wa upinzani wa nchi hiyo. Muda mfupi baada ya hapo muungano wa upinzani wa Venezuela ulitangaza kwamba umemteua Henrigue Capriles ambaye alishindwa na Chavez katika uchaguzi wa mwezi Oktoba kuwa mgombea wa upinzani katika kinyang'anyiro cha rais.
Inaonekana kuwa Maduro ana nafasi nzuri ya ushindi katika uchaguzi huo, kutokana na uungaji mkono mkubwa wa chama tawala hasa baada ya kufariki dunia Chavez. Harakati na uadui wa kisiasa umeanza kushuhudiwa masaa kadhaa baada ya mazishi ya Chavez nchini Venezuela ambapo wapinzani wanaoungwa mkono na madola ya kibeberu ya Magharibi wanadai kuwa Maduro ameapishwa kinyume na katiba ya nchi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO