Sunday, March 10, 2013

WAMISRI WATAKIWA KUHESHIMU SHERIA ZA NCHI


Msemaji wa serikali ya Misri amesisitiza udharura wa kuheshimiwa katiba ya nchi hiyo. Alaa al Hadidi msemaji wa Waziri Mkuu wa Misri sambamba na kusisitiza udharura wa watu wote kuheshimu sheria na katiba ya nchi hiyo amewataka Wamisri, kutanguliza mbele maslahi ya kitaifa kuliko ya makundi yao binafsi na kujiepusha kuharibu miundombinu na majengo nchini humo. Al Hadidi amesema, haki ya kujieleza na kuandamana kwa amani nchini Misri inapaswa kuheshimiwa lakini wakati huo huo ameyataka makundi yote ya nchi hiyo kuacha kuharibu miundombinu na kuchoma moto majengo ya serikali na yasiyokuwa ya serikali.
Kwa siku kadhaa miji tofauti ya Misri imeshuhudia vurugu na makabiliano kati ya wanaounga mkono serikali na wanaoipinga, huku baadhi ya vikundi vikichoma moto maeneo ya umma na majengo ya serikali.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO