Saturday, March 02, 2013

WAANDAMANAJI WAPINGA KUBOMOLEWA UKUTA WA BERLIN

Waandamanaji nchini Ujerumani, jana walijaribu kuzuia kubomolewa kwa sehemu ya mwisho iliyobakia ya Ukuta wa Berlin, kwa ajili ya kujenga nyumba za kifahari. Eneo la umbali wa kilomita 1.3 la ukuta huo uliochorwa unaojulikana kama East Side Gallery ulitangazwa kama mnara wa kihitoria mwaka 1992 na tangu wakati huo umekuwa kivutio kikubwa kwa watalii. Viongozi wa Kikomunisti wa iliyokuwa Ujerumani Mashariki, waliujenga ukuta huo mwaka 1961. Sehemu kubwa ya ukuta huo ilibomolewa Novemba mwaka 1989. Waandamanji hao wamemtaka Meya wa Mji wa Berlin kusitisha shughuli za kuuvunja ukuta huo wakisema kuwa historia ya mji huo inafutika. Ukuta huo wenye urefu wa mita 3.6 uliigawa Berlin kwa miaka 28. Inakadirwa kuwa Wajerumani 1,000 wa Mashariki waliuawa walipokuwa wakijaribu kukimbilia eneo la Magharibi baada ya ukuta huo kujengwa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO