Saturday, March 02, 2013

SENETA WA MAREKANI AMUUNGA MKONO KIONGOZI WA IRAN

Seneta wa zamani wa Marekani amesema kuwa, Ayatullahil Udhma Khamanei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni shakhsia aliye na sifa kamili za kuwa kiongozi wa kidini na mwenye ushawishi mkubwa kwa wafuasi wa madhehebu ya Shia duniani. Mike Gravel seneta wa zamani wa jimbo la Alaska nchini Marekani amesema kuwa, Marekani inapaswa kuchukua somo na funzo kutokana na vigezo vya kisiasa vya Iran. Gravel ameongeza kuwa, amevutiwa mno na maneno ya kimantiki yaliyotolewa na Ayatullah Khamenei pale aliposema kuwa, 'Qurani Tukufu inapiga marufuku utumiaji wa bomu la atomiki'. Mike Gravel aliyewahi kuwa seneta wa Marekani kwa vipindi viwili, alijipatia umashuhuri mwaka 2008 baada ya kufichua nyaraka za siri za Wizara ya Ulinzi ya Marekani.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO