Saturday, March 02, 2013

WATURUKI WAPINGA UJIO WA KERY

Maandamano dhidi ya Marekani yamefanyika nje ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Uturuki huko Ankara katika kupinga ziara rasmi ya John Kerry Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani nchini humo. Kerry alielekea Uturuki kwa ajili ya kuratibu mipango ya kuwaunga mkono wapinzani wa serikali ya Syria. Polisi wa Uturuki jana walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakijaribu kuvunja vizuizi vya askari usalama karibu na ofisi ya Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Wafanya maandamano walikuwa wamebeba mabango yaliyosema "Kerry ondoka nchini kwetu" huku mengine yakilaani hatua ya madola ya kibeberu ya kuanzisha vita dhidi ya nchi nyinginezo. John Kerry ambaye anafanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi akiwaWaziri wa Mambo ya Nje wa Marekani jana aliwasili Ankara Uturuki akiwa katika mfululizo wa ziara yake ya kuzitembelea nchi tisa za Ulaya na Mashariki ya Kati lengo likiwa ni kutafuta uungaji mkono kwa makundi ya wapinzani wanaopigana dhidi ya serikali ya Rais Bashar al Assad wa Syria. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani tayari amewasili Cairo mji mkuu wa Misri.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO