Tuesday, March 19, 2013

WAZIRI MKUU WA MPITO ACHAGULIWA BARAZA TAIFA LA SYRIA

Baraza la Taifa la Syria limemchagua Ghassan Hitto kuwa waziri mkuu wake kwa kwanza wa mpito. Hitto ambaye ni mfanyabiashara na mwanaharakati wa Kiislamu, aliishi nchini Marekani kwa miongo kadhaa. Mwanasaiasa huyo anaongoza kitengo cha msaada wa kibinaadamu kwenye muungano wa upinzani, chenye makao yake nchini Uturuki. Atakuwa na jukumu la kuunda serikali ya mpito ya Syria, itakayosimamia maeneo yanayodhibitiwa na waasi. Baraza la Taifa la Syria jana  lilimchagua Hitto , wakati wa mkutano wao uliofanyika mjini Istanbul, Uturuki.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO