Tuesday, March 19, 2013

MKAGUZI WA SILAHA ASEMA MAREKANI ILIFANYA UNYAMA IRAQ


Hans Blix Mkuu wa zamani wa ukaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amesema kuwa, shambulio la Marekani na washirika wake dhidi ya Iraq mwaka 2003  lilikuwa kwa kimakosa. Blix amesema kuwa, wakaguzi wa Umoja wa Mataifa hawakushuhudia silaha za mauaji ya halaiki  nchini Iraq, lakini Donald Henry Rumsfeld Waziri wa Ulinzi wa Marekani katika kipindi kile alidai kwamba Washington wana ushahidi tosha kwamba utawala wa Iraq ulikuwa unamiliki silaha za mauaji ya halaiki.
Amesema kuwa, Washington hadi leo hawajathibitisha madai yao hayo. Marekani na washirika wake waliivamia Iraq tarehe 20 Machi 2003 kwa kisingizio kwamba serikali ya dikteta Saddam Hussein inamiliki silaha za maangamizi.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, utawala wa Saddam Hussein uliangushwa baada ya kupita wiki tatu tokea kuanza vita hivyo, na ilipofika 30 Disemba 2006  dikteta huyo wa zamani wa Iraq aliuawa kwa kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kutenda jinai dhidi ya binadamu na jinai nyingine za kivita.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO