Harakati ya Mupambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imekosoa vikali pendekezo la ulaghai la Waziri wa Mambo ya Nje wa Canad John Baird la kutaka kuwapa wakimbizi wa Palestina uraia wa Canada. John Baird Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada hivi karibuni alisema kuwa nchi yake inaweza kuwapa makazi na uraia wakimbizi wa Kipalestina 120,000.
Duru mpya ya harakati za serikali za Magharibi kwa ajili ya kuzuia haki ya kurejea wakimbizi wa Palestina katika ardhi zao imeanza huku utawala wa Kizayuni pia ukiwa umechukua hatua mpya katika Umoja wa Mataifa ili kufuta haki ya kurejea wakimbizi wa Palestina katika ardhi zao, haki ambayo tayari imetambuliwa rasmi na umoja huo. Katika fremu hiyo utawala wa Kizayuni wa Israel unafanya kila linalowezekana ili Umoja wa Mataifa upige marufuku matumizi ya neno "wakimbizi wa Palestina" kwa ajili ya kizazi kipya cha Wapalestina wanaoishi katika nchi nyingine na kwa hiyo upoteze haki ya Wapalestina ya kurejea katika ardhi zao za asili. Katika kalibu hiyo utawala wa Kizayuni umeandaa ajenda ya kubadili sheria zinazohusiana na wakimbizi wa Palestina kupitia Umoja wa Mataifa na taasisi zenye mfungamano na umoja huo na kwa njia hiyo utawala huo ghasibu ufanikiwe kufuta kabisa neno "mkimbizi" miongoni mwa Wapalestina uliowafukuza katika makazi yao.
Duru hii mpya ya njama za utawala wa Kizayuni na serikali za Magharibi inayofanyaka sambana na harakati za Marekani za kufufua mwenendo eti wa amani ya Mashariki ya Kati ni ishara ya njama kubwa zinazotekelezwa na nchi za Magharibi dhidi ya wananchi madhlumu wa Palestina. Siasa za kuwafukuza raia wa Palestina katika nchi yao kwa shabaha ya kuimarisha nafasi ya utawala ghasibu wa Israel katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina zilikuwa katika ajenda ya utawala huo haramu tangu awali, jambo ambalo limewafanya mamilioni ya Wapalestina kuwa wakimbizi.
Kuweko wakimbizi zaidi ya milioni tano na nusu wa Kipalestina wanaoishi katika nchi mbalimbali, idadi ambayo inaunda sehemu kubwa ya wakimbizi duniani, ni kielelezo cha maafa makubwa yaliyosababishwa na utawala wa Kizayuni kwa raia wa Palestina. Hii ni katika hali ambayo utawala wa Kizayuni wa Israel unapinga wazi wazi maazimio nambari 194, 302 na 512 ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa yanayosisitiza juu ya haki ya kurejea wakimbizi wa Palestina katika ardhi zao na kulipwa fidia. Nchi za Magharibi khususan Marekani pia ambayo ni muungaji mkono mkuu wa hali na mali wa utawala ghasibu wa Israel daima zimekuwa zikishirikiana na Israel kupanga njama za kufutilia mbali haki ya kurejea wakimbizi wa Palestina katika ardhi zao.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO