Saturday, April 13, 2013

OIC YATAKA KUONDOLEWA VIZINGITI UKANDA WA GHAZA

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imetaka kufunguliwa haraka vivuko vya mpakani mwa Ukanda wa Gaza huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Ekmeleddin İhsanoğlu ametaka kufunguliwa haraka vivuko vya mpakani mwa Ukanda wa Gaza na kukomeshwa sera za kuwaadhibu raia kwa halaiki kupitia ufungaji wa makusudi na wa muda mrefu wa kivuko cha Karam Abu Salim. Katibu Mkuu wa OIC amezitaka jumuiya za kimataifa na taasisi za kutetea haki za binadamu ziushinikize utawala haramu wa Israel ili uvifungue vivuko vya mpakani mwa Ukanda wa Gaza. Huku akiashiria kuwa Israel ni utawala pekee unaotumia visingizio hewa vya kiusalama kuhalalisha hatua yake kuwaadhibu watu kwa halaiki, Ekmeleddin İhsanoğlu amesema suala hilo linaipa jamii ya kimataifa jukumu kubwa la kuitaka ichukue hatua ya kukomesha ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza. Inakadiriwa kuwa tangu ulipoanza mwaka huu wa 2013 hadi sasa Ukanda wa Gaza umepata hasara ya jumla ya dola milioni 700 za kimarekani kutokana na hatua ya utawala haramu wa Israel ya kukifunga mara kwa mara kivuko cha Karam Abu Salim

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO