Wednesday, April 24, 2013

JOHN KERY ATAKA NATO KUINGIALIA KATI SYRIA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry ameutaka Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) kujiandaa kuingia kijeshi nchini Syria iwapo mambo 'yatakwenda upogo'. Kerry amewaambia Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa NATO mjini Brussels kwamba, muungano wao lazima uwe tayari kujibu shambulio lolote litakalofanywa na jeshi la Syria kwa kutumia silaha za kemikali. Marekani imekuwa ikitoa madai ya uongo kwamba serikali ya Syria imetumia silaha za kemikali dhidi ya raia na makundi ya wapinzani lakini ukweli unaonyesha kwamba yumkini huenda wapinzani wenye kubeba silaha ndio waliotumia silaha hizo kwa msaada wa Marekani. Licha ya tuhuma hizo, Washington imeshindwa kutoa ushahidi kuhusu jambo hilo. Weledi wa mambo wanaamini kuwa, Marekani sasa inajaribu kutumia muungano wa NATO kufikia malengo yake haramu huko Syria. Hii ni katika hali ambayo, Rais Bashar Asad ameahidi kuendelea kupambana vikali na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani na waitifaki wake.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO