Wednesday, April 24, 2013

NIGER YAKANUSHA KUPAMBANA NA BOKO HARAM

Waziri wa Ulinzi wa Niger amesema kuwa, jeshi la nchi hiyo halikushiriki kwenye mapigano makali yaliyojiri wiki iliyopita baina ya jeshi la Nigeria na wanamgambo wa kundi la Boko Haram katika eneo la mpaka wa nchi hizo mbili.
Muhammad Karidio Waziri wa Ulinzi wa Niger amesisitiza kuwa, majeshi ya Nigeria ndio yaliyotekeleza operesheni hiyo ya kijeshi. Waziri wa Ulinzi wa Niger amesema kuwa, kundi la Boko Haram sio tishio la moja kwa moja kwa usalama wa Niger japokuwa Niamey inatoa mashirikiano kwa serikali ya Abuja ya kuliangamiza kundi hilo. Kwenye mapigano yaliyojiri tarehe 19 Aprili, watu wasiopungua 187 waliuawa  katika  eneo la  Baga lililoko Maiduguri, karibu na mpaka wa nchi za Niger na Cameroon.
Afisa mmoja mwandamizi wa jeshi la Niger amesema kuwa, wanamgambo wa Boko Haram tarehe 16 mwezi huu walishambulia doria za majeshi ya Nigeria na Niger katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO