Jordan leo imefungua kambi ya pili ya wakimbizi wa Syria baada ya Umoja wa Mataifa kusema kuwa idadi ya wanaotafuta hifadhi katika nchi hiyo inatarajiwa kupanda mara tatu zaidi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Msemaji wa serikali kuhusu masuala ya wakimbizi wa Syria amesema kundi la kwanza la wakimbizi 106, ambao walikuwa miongoni mwa wakimbizi 1,306 waliovuuka mpaka saa za usiku, limehamishwa hadi kambi mpya ya Mrigeb al-Fuhud. Kambi hiyo ina hospitali na shule na ina uwezo wa kuwahifadhi wakimbizi 5,500. Aidha kambi hiyo iliyogharimu dola milioni 9.8 iligharamiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu. Kwa sasa kambi hiyo itawachukua wajane, watoto na familia zisizo na wanaume. Kuna mipango ya kuipanua kambi hiyo ili iweze kuwahifadhi watu 30,000.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO