Kamisheni Huru ya Uchaguzi nchini Ivory Coast imetangaza kuwa, kundi la watu katika eneo la kusini mwa Abidjan hapo jana lilivamia na kupora masanduku ya kura, wakati likiendelea zoezi la kuhesabu kura zilizopigwa katika uchaguzi wa mabaraza ya miji nchini humo.
Msemaji wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Ivory Coast amesema kuwa, karibu watu 200 walivamia eneo la Treichville na kutoweka na makaratasi ya kura, taarifa za uchaguzi na hali kadhailka masanduku ya kupigia kura, huku askari wa usalama waliokuwepo kwenye eneo hilo wakishindwa kuzuia uhalifu huo. Amesema kuwa, hadi sasa haijajulikana ni mrengo gani wa kisiasa uliopanga njama hizo za kupora masanduku ya kura.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO