Monday, April 15, 2013

MPINZANI WA MADURO APINGA MATOKEO YA URAIS

Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela, Henrique Capriles, ameyalalamikia matokeo ya uchaguzi wa jana wa urais yaliyompa ushindi Nicolas Maduro. Capriles, ambaye pia ni gavana wa jimbo la Miranda, anataka zoezi la kuhesabu kura lirudiwe upya. Katika uchaguzi huo, Maduro ameshinda kwa kupata asilimia 50.76 ya kura zilizopigwa, huku Capriles akiwa amepata asilimia 49.07. Hata hivyo, Maduro, ambaye alikuwa mrithi wa rais wa taifa hilo, Hugo Chavez, amesema amezungumza na Capriles kwa njia ya simu na amemwambia mpinzani wake huyo lazima ayatambue matokeo ya uchaguzi, kama ambavyo wagombea hao waliahidi kufanya hivyo wakati wa kampeni. Kwa upande mwengine, Maduro amesema hana tatizo na kurejewa kwa hesabu ya kura.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO