Monday, April 15, 2013

ISRAEL YAPANGA KUHARIBU USHIRIKIANO WA SUDAN MBILI

Gazeti moja la utawala wa Kizayuni limekiri kuwa utawala huo unajaribu kila unaloweza kuzusha hitilafu kati ya Sudan na Sudan Kusini. Gazeti la Malam limeripoti kuwa, Israel ina wasiwasi na kumalizika hitilafu kati ya nchi mbili za Sudan. Gazeti la Malam limemnukuu Moshe Yaalon, Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni na kuandika kama ninavyomnukuu: "Sisi hatupaswi kutoa mwanya wa kumalizika hitilafu kati ya Sudan na Sudan Kusini." Gazeti la Malam limeandika pia kuwa, Waziri wa Vita wa Israel Moshe Yaalon amekiri kuwa Tel Aviv inawasaidia waasi katika eneo la Darfur la magharibi mwa Sudan na kueleza kuwa, Israel haipaswi kutoa mwanya wa kupatiwa ufumbuzi mgogoro wa jimbo la Darfur, bali utawala wa Kizayuni unapaswa kuchochea moto wa vita katika eneo hilo usizime hata sekunde moja.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO