Spika wa Bunge nchini Bahrain, Khalifa bin Ahmed Al Dhahrani amefichua njama za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi za kuiweka Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon katika orodha yake ya makundi ya kigaidi. Dhahrani amehoji juu ya uhusiano wa nchi yake na taifa la Lebanon endapo hatua hiyo itachukuliwa. Hata hivyo spika huyo wa bunge nchini Bahrain ametetea hatua hiyo kwa kudai kama ninavyo mnukuu, "Uhusiano na taifa la Lebanon hautabadilika kama ambavyo pia uhusiano kati ya nchi wanachama hautabadilika." Mwisho wa kunukuu. Ameongeza kuwa, wanachama wa Baraza la Ushirikiano ya Ghuba ya Uajemi wanalijadili kwa kina suala hilo. Kuhusiana na vizingiti vinavyozuia maelewano ya nchi wanachama wa baraza hilo Dhahrani amesema kuwa, kuna udharura wa nchi hizo kumaliza tofauti zao na kufikia maelewano. Hii ni katika hali ambayo kwa mara kadhaa serikali ya Manama imekuwa ikitoa tuhuma zisizo na msingi wowote wala ushahidi kwamba, Harakati hiyo ya Hizbullah imekuwa ikichochea maandamano ya wananchi nchini Bahrain. Viongozi wa Hizbullah wamekuwa wakikanusha vikali madai hayo. Hatua hiyo inakuja huku hata Umoja wa Ulaya (EU) umekataa kuiweka harakati hiyo katika orodha ya makundi ya kigaidi na kusisitiza kuwa, Harakati ya Hizbullah ni chama kamili cha kisiasa ambacho hakifai kuitwa cha kigaidi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO