Tuesday, April 09, 2013

TETEMEKO KUBWA LAATHIRI KUSINI MWA IRAN


Tetemeko la ardhi  lenye nguvu ya 6.1 kwenye kipimo cha Richter limetikisa eneo la Kaki karibu mji wa Bushehr kusini mwa Iran. Shirika la Habari la Fars limesema  watu 32 wamepoteza maisha na wengine  850 kujeruhiwa katika zilizala hiyo.
Taasisi ya Kupimatetemeko ya  Iran imesema  tetemeko hilo limejiri leo Jumanne alasiri huko Kaki kilomita tisini kusini mwa Bushehr na kina chake kilikuwa kilomita 12 ndani ya ardhi. Zilizala hiyo pia imehisika katika nchi za Ghuba ya Uajemi za Kuwait, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu.
Kituo cha Kuzalisha Nishati ya Nyuklia cha Bushehr hakikuharibiwa hata kidogo na zilizala hiyo. Shirika la Urusi la Atomstroyexport ambalo limejenga kituo hicho cha nyuklia limetoa taarifa na kusema tanuri nyuklia ya Bushehr iko katika hali ya kawaida kabisa. Iran  iko katika eneo ambalo hukumbwa na mitetemeko ya ardhi mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO