Waziri wa Viwanda na Biashara wa Misri amesema kuwa, Russia inakusudia kuisaidia Misri katika kutekeleza miradi ya nishati ya nyuklia nchini humo. Hatim Swaleh ameongeza kuwa, makubaliano ya Russia ya kuisaidia Misri katika nishati ya nyuklia yamefanyika katika safari iliyofanywa wiki iliyopita na Rais Muhammad Morsi wa Misri nchini Russia. Ameongeza kuwa, Russia itaisaidia Misri katika suala la utafiti kwenye kinu cha nyuklia cha al Dhwaba'a na ustawishwaji wa shughuli za kinu cha kiutafiti cha an Shaasw. Waziri wa Viwanda na Biashara wa Misri amesema kuwa, serikali ya Cairo inataka kupiga hatua mbele kuelekea kwenye mpango wa kujipatia nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO