Tuesday, April 23, 2013

ALI ZIDAN: HATUTOOMBA MSAADA KUTOKA NATO


Waziri Mkuu wa Libya amesema kuwa, nchi yake kamwe haitaomba msaada wa vikosi vya NATO kwa ajili ya kuingilia mgogoro wa ndani nchini humo.
Ali Zidan amekadhibisha vikali uvumi juu ya uwezekano wa kuingilia kijeshi vikosi vya Nato nchini Libya na kusisitiza kuwa, uvumi huo unatolewa kwa shabaha ya kutia doa utendaji wa serikali ya Libya.
Akizungumza na mkuu wa jeshi la polisi na makamanda wa jeshi hilo mjini Tripoli, Zidan amongeza kuwa, wananchi wa Libya wameshuhudia utendaji wa serikali yake na wala hakuna siri yoyote inayofichwa na serikali ya nchi hiyo. Amesisitiza kuwa, serikali ya Libya haijaomba na wala haitaomba msaada wowote kutoka Nato, na hata kama litatolewa, basi bila shaka awali  linapasa kupata baraka za Kongresi ya Taifa la Libya.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO