Kampeni za Rais Barack Obama wa Marekani za kukabiliana na matumizi holela ya silaha zimepata pigo baada ya Bunge la Seneti kupinga mpango wa kuzidisha ukaguzi wa cheki kwa wanunuzi wa silaha. Bunge la Seneti halikupitisha mpango huo uliowasilishwa kwa lengo la kuzidisha uchunguzi wa cheki na kuwabana wanunuzi silaha baada ya kushindwa kupata kura za kutosha, hatua iliyoipa ushindi lobi inayounga mkono matumizi ya silaha ya Marekani. Rais Obama ameonyesha kusikitishwa na suala hilo na kulaumu bunge hilo kwa kusema kuwa uamuzi huo ni aibu kwa Marekani.
Mpango huo ulipendekezwa kwa lengo la kukabiliana na matumizi holela ya silaha hasa baada ya mtu mmoja kuua wanafunzi 20 katika shule ya msingi mjini Newtown Disemba mwaka jana. Inakadiriwa kuwa, kila mwaka takriban watu 30,000 huuawa kutokana na matumizi holela ya silaha nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO