Friday, May 10, 2013

ANUSURIKA KATIKA AJLIA YA GHOROFA NA KUKAA CHINI YA KIFUSI KWA SIKU 17, 1000 WAFARIKI

Mwanamke  mmoja  ambaye  alikuwa  katika  kifusi  cha  nyumba  ya ghorofa  tisa  iliyoporomoka  siku  17  zilizopita  ameokolewa  akiwa hai  leo, wakati  ambapo  idadi  ya  waliofariki imepita  kiasi  ya  watu 1,000. Reshma  amenusurika , akiwa  katika  hali  nzuri, kwa  kula chakula  kilichokaushwa  ambacho  kilikuwa  katika  eneo  hilo  na kunywa  maji  aliyokuwa  nayo. Aligunduliwa   akiwa  katika  ghorofa ya  pili  ya  jengo  hilo  la  ghorofa  tisa   la Rana  Plaza, ambako waokoaji  walikuwa  wakilenga  kutoa  miili  ya  watu  waliofariki, na sio  kupata  mtu  aliye  hai, kwa  muda  wa  wiki  mbili  zilizopita.
Reshma  amekiambia  kituo  cha  televisheni  cha  Somoy  akiwa hospitalini  kuwa  alikuwa  akiwasikia  waokoaji  kwa  siku  kadha  na alijaribu  kupiga mahali  alipo kwa  fimbo  ili  kuwajulisha  kwamba  yu hai.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO