Friday, May 10, 2013

WAMISRI WAANDAMANA KUTETEA QUDS


Mamilioni ya wananchi wanafanya maandamano leo mbele ya Chuo Kikuu cha al Azhar wakitetea Quds Tukufu inayokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.
Jumuia na taasisi 11 za Misri zimetayarisha maandamano hayo yatakayofanyika kwa ajili ya kulaani hujuma ya Wazayuni wa Israel dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa na kutiwa nguvuni Mufti wa Quds.
Aiman A'mir ambaye ni mratibu wa Muungano wa Mapinduzi ya Januari 25 amesema maandamano ya leo yanafanyika kupinga uvamizi wa utawala haramu wa Israel dhidi ya Msikiti wa al Aqsa na kutiwa nguvuni Mufti wa Quds, wasomi wengine kadhaa na vijana wa Kipalestina na vilevile kulaani shambulizi la Israel dhidi ya Syria na jinai zinazofanywa dhidi ya Waislamu nchini Myanmar.
Katika upande mwingine Mkurugenzi wa Kamati ya Quds katika Jumuiya ya Madaktari wa Kiarabu Jamal Abdu Salaam amelaani uhalifu unaofanywa na Israel huko Quds tukufu na kusema hatua za utawala huo haramu za kuwazuia Waislamu an Wakristo kutekeleza ibada zao katika mji huo mtakatifu na ubaguzi unaopaswa kupigwa vita.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO