Friday, May 10, 2013

UMOJA WA WANAZUONI TANZANIA WATOA TAMKO JUU YA ULIPUAJI WA ARUSHA


Taasisi ya Muungano wa Wanazuoni wa Kiislamu nchini Tanzania Hayatul Ulama imewataka Watanzania kutolihusisha suala la hivi karibuni la mripuko wa bomu mjini Arusha na taasisi, kikundi, madhehebu, dini na wala chama chochote na waviachie vyombo husika vifanye uchunguzi wake na hatimae mhusika au wahusika waweze kufikishwa katika vyombo vya kisheria.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran imepata nakala yake, taasisi ya Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania kupitia mwenyekiti wake Sheikh Sulaiman Amran Kilemile pia imewataka Waislamu wote nchini humo kuwa watulivu na kamwe wasichokozeke na matamshi yanayotolewa na baadhi ya watu au baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vina malengo yao yasiyo bayana.
Vile vile taasisi hiyo ya Hayatul Ulama imevitaka vyombo hivyo kuweka wazi matokeo  ya uchunguzi wa tukio hilo na yanayofanana na hilo kama yale ya Zanzibar, ili kuondoa hisia zinazoweza kusababisha chuki na kudhaniana vibaya kati ya watu wa dini tofauti nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO