Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa, askari 3000 wakulinda amani wa Umoja wa Afrika waliotumwa Somalia, wameuawa tangu mwaka 2007 hadi sasa. Hayo yamesemwa leo na Jan Eliasson Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa, askari hao walipoteza maisha yao wakiwa wanafanya juhudi za kumaliza hali ya machafuko na ukosefu wa amani huko nchini Somalia. Jan amezishukuru nchi zote zilizokubali kubeba gharama yoyote kwa kutuma askari wake nchini humo. Aidha Jan Eliasson amesema kuwa wameshtushwa na idadi hiyo ya askari 3000 waliouawa Somalia katika kipindi hicho. Karibu askari elfu 17 wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika AMISOM wako nchini Somalia tangu mwaka 2007. Wengi wa askari hao wanatoka Burundi, Uganda, Kenya, Sierra Leone na Djibouti. Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, askari wengi waliouawa nchini Somalia ni wa Burundi na Uganda.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO