Rais Muhammad Mursi wa Misri amesema kuwa, nchi yake inakusudia kujiunga na nchi wanachama wa kundi la nchi zinazoinukia kwa kasi kiuchumi BRICS. Mursi ambaye amesema hayo mjini Brasilia, Brazil wakati alipofanyiwa mahojiano na televisheni moja ya nchi hiyo na kuongeza kuwa, nchi yake iko tayari kwa ajili ya kujiunga na kushirikiana na kundi hilo la BRICS. Rais wa Misri ambaye aliapishwa kuwa rais wa nchi hiyo mwezi Juni mwaka jana amesisitiza pia kuwa viwanda vya Misri sasa vinafufuka. Taarifa zinadai kuwa uchumi wa Misri ulikuwa mwaka 2012 lakini harakati za mapinduzi ya wananchi wa nchi hiyo dhidi ya utawala wa dikteta Hosni Mubarak, zimepelekea uchumi wa nchi hiyo uporomoke kutokana na machafuko na ukosefu wa usalama. Aidha hali hiyo imepelekea kupungua hazina ya fedha za kigeni na hivyo kusababisha hasara kubwa katika sekta za utalii na uwekezaji nchini Misri. Hata hivyo Rais Mursi amesisitiza kuwa, nchi yake ina ushawishi na uwezo mkubwa katika eneo lake.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO