Wednesday, May 22, 2013

ASKARI WA MAREKANI WAFYATULIA RISASI WAFUNGWA WA GUANTANAMO

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni, inaonyesha kuwa mbali na kuteswa kwa adhabu kali tofauti, wafungwa wa jela ya Guantanamo, hufyatuliwa pia risasi na askari wa jela hiyo. Televisheni ya Russia Today imeonyesha mkanda wa video uliosambazwa na mawakili wa wafungwa wa jela hiyo ya kutisha ambao unawaonyesha wafungwa hao wakifyatuliwa risasi na askari wa Marekani. Ramzi Kassem mmoja wa mawakili wa wafungwa wa jela hiyo, amenukuliwa akisema kuwa, tukio la tarehe 13 April mwaka huu linaonyesha wazi kuwa seli za wafungwa hao zinashambuliwa kwa risasi. Amesema katika tukio hilo mfungwa Muadh al-Aawi mwenye umri wa miaka 35, alipatwa na mojawapo ya risasi hizo. Pamoja na al-Aawi kupigwa risasi, alicheleweshwa hakupatiwa matibabu. Viongozi wa Marekani ikiwemo Wizara ya Sheria, wamekiri kujiri tukio hilo. Muadh al-Aawi ni miongoni mwa wafungwa wa jela ya Guantanamo ambaye hakujathibitishwa tuhuma zozote dhidi yake. Baada ya Rais Barack Obama wa Marekani kuingia madarakani, aliahidi kuifunga jela hiyo, lakini hajatekeleza ahadi hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO