Askari wa Algeria kwa kushirikiana na kikosi maalumu cha kulinda mpaka wa nchi hiyo, wamepambana na magaidi waliokuwa wanakusudia kuvuka mpaka wa Tunisia kuingia nchini humo. Kiongozi mmoja wa usalama wa Algeria amesema kuwa, mapigano hayo yalijiri usiku wa jana katika eneo la Buque Fella lililoko kusini mwa mkoa wa al-Wadi kilometa 600 kusini mashariki mwa Algeria, kati ya magaidi hao na askari jeshi kwa kushirikiana na kikosi maalumu cha kulinda mpaka nchini humo. Afisa huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa yeye siye msemaji wa jeshi, amesema kuwa, magaidi hayo yalikuwa yanakusudia kupenya mpaka na kuingia eneo la jangwani nchini Algeria. Katika operesheni hiyo, gaidi mmoja ameuawa na wengine wawili wametiwa mbaroni. Afisa huyo amesema kuwa, katika oparesheni hiyo, silaha kadhaa na zana nyingine za magaidi hao kikiwemo chombo kimoja cha mawasiliano kilichotengezwa Marekani zimedhibitiwa na jeshi la Algeria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO