Ban Ki moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameingiwa na wasiwasi na kuchukizwa na misimamo ya kuchupa mipaka ya Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Eduardo del Buey Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Ban Ki moon amechukizwa na misimamo iliyochukuliwa na Netanyahu ya kutaka kuweka ukomo wa kuingia Wapalestina kwenye eneo la Masjidul Aqswa mashariki mwa Baitul Muqaddas. Ameongeza kuwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel na Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina juu ya kuhuisha mwenendo wa mazungumzo ya amani kati ya pande hizo mbili. Inafaa kuashiria hapa kuwa, kwa zaidi ya miongo sita sasa utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukifanya njama mbalimbali dhidi ya Masjidul Aqswa ikiwa ni pamoja na kuchimba mashimo na njia za chini ya msikiti huo kwa lengo la kuliharibu eneo hilo tukufu la Waislamu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO