Thursday, May 16, 2013

WATU WENYE SILAHA WATEKA POLISI NA WANAJESHI WA MISRI

Watu wasiojulikana waliokuwa na silaha wamewateka nyara maafisa watatu wa polisi na wanajeshi wanne mjini Sinai nchini Misri leo.Maafisa wa usalama wamesema wenzao walikuwa wakisafiri kwa mabasi madogo kuelekea mji mkuu Cairo wakati waliposimamishwa na watu waliokuwa na bunduki katika eneo la Al Wadi Akhadar lililoko kaskazini mwa Sinai.Maafisa hao watatu waliotekwa nyara wanatokea kikosi kikuu cha usalama kilicho na idara katika wizara ya mambo ya ndani kinachotumika kutuliza ghasia na wanne ni kutoka jeshini.Mpaka sasa watekaji nyara hao hawajatoa matakwa yoyote lakini viongozi wa jamii ya  Wabedouin wameitwa kuwa wapatanishi kati ya utawala na watekaji nyara hao.Duru za jamii hiyo  zinaarifu kuwa inaaminika watekaji nyara hao wanataka kuachiliwa kwa wafungwa fulani.Wimbi la utekaji nyara ambao huwa haudumu kwa zaidi ya saa 48 lilianza Sinai baada ya uasi uliomngoa madarakani Rais Hosni Mubarak mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO