Wednesday, May 22, 2013

NIGERIA KUWAACHIA WATUHUMIWA WA UGAIDI WANAWAKE

Habari kutoka Nigeria zinasema kuwa serikali ya nchi hiyo imetangaza kwamba itawaachia huru wafungwa wote wanawake wanaoshikiliwa kwa tuhuma za ugaidi. Pia baadhi ya watu wanaotuhumiwa kuhusika na ugaidi wataachiwa huru. Wachambuzi wengi wanaiona hatua hiyo kama njia ya kuwapoza wanamgambo wa Boko Haram ambao huko nyuma walikuwa wameitaka serikali kuwaachia huru watuhumiwa wa ugaidi wakiwemo wanawake. Hata hivyo serikali haikusema iwapo hatua yake hiyo ni katika fremu ya kutekeleza matakwa ya Boko Haram. Fauka ya hayo, serikali ya Nigeria imesema itaendelea na oparesheni yake ya kijeshi kaskazini mwa nchi ili kukabiliana barabara na makundi ya wanamgambo hususan kundi la Boko Haram. Shirika la Msalaba Mwekundu limesema kuwa, hadi sasa zaidi ya watu 2000 wamekimbia makazi yao tangu jeshi lianzishe oparesheni kali kaskazini mwa nchi wiki moja iliyopita.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO