Sunday, May 05, 2013

ISRAEL YASHAMBULIA KITUO CHA KIJESHI SYRIA


Utawala wa Kizayuni wa Israel umetekeleza hujuma ya angani dhidi ya kituo cha utafiti wa kijeshi nje kidogo ya mji mkuu wa Syria, Damascus.
Serikali ya Syria imethibitisha kujiri shambulizi hilo ambalo linakuja baada ya utawala wa Kizyauni kusema ulitekeleza hujuma nyingine nchini Syria siku ya Ijumaa.
Televisheni ya Press TV imesema hujuma hiyo dhidi ya Syria iliidhinishwa Alkhamisi usiku katika kikao cha siri cha Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni na maafisa wa ngazi za juu wa usalama.
Wakati huo huo siku ya Jumamosi Rais Bashar al-Assad wa Syria alitembelea Chuo Kikuu cha Damascus na kuzindua kumbukumbu ya mashahidi wa chuo hicho. Akizungumza katika halfa hiyo Rais Assad amelishukuru taifa la Syria kwa kusimama kidete mbele ya njama za maadui. Serikali ya Syria inasema magaidi nchini humo wanapata himaya ya nchi za Magharibi hasa Marekani na vile vile utawala haramu wa Israel pamoja na waitifaki wao katika eneo ambao ni Qatar, Saudi Arabia na Uturuki. Magaidi wanaoipinga serikali ya Syria wametekeleza mauaji dhidi ya raia ikiwa ni pamoja na kutumia silaha za sumu vitani.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO