Sunday, May 12, 2013

JALILI AJITOSA UCHAGUZI WA IRAN

Mjumbe mkuu wa usuluhishi wa mzozo wa nuklea wa Iran Saeed Jalili amejiandikisha kugombania urais katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika hapo tarehe 14 mwezi wa Juni.Jalili ambaye ni mkongwe wa vita kati ya Iran na Iraq vya miaka ya 1980 , tangu  2007 amekuwa akiliongoza Baraza Kuu la Taifa la Usalama nchini Iran na anahesabiwa kuwa ni muhafidhina wa msimamo mkali alie karibu na Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.Ugombea wa Jalili lazima uidhinishwe na baraza la masheikh na majaji wa kihafidhina linalojulikana kama Baraza la Walezi ambalo linatarajiwa kutowa orodha yake ya mwisho ya wagombea walioidhinishwa kugombea urais katika kipindi kisichozidi siku kumi.Habari za hivi punde zinasema naye Rais wa zamani wa nchi hiyo Akbar Hashemi Rafsanjani amejiandiksha dakika za mwisho kugombania wadhifa huo wa urais.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO