Jeshi la Afghanistan litachukua jukumu la kuongoza operesheni za kusimamia usalama nchini humo katika kipindi cha miezi miwili ijayo huku majeshi ya jumuiya ya kujihami ya Nato yakijiondowa.Msemaji wa wizara ya ulinzi Zahir Azimi amesema jeshi la nchi hiyo liko tayari kuongoza operesheni hizo.Tangazo hilo linakuja huku kundi la wanamgambo la Taliban likitangaza mwanzo wa msimu mpya wa mashambulio dhidi ya majeshi ya kigeni na ya Afghanistan pamoja na wafanyakazi wa umma.Mjini London wizara ya ulinzi ya Uingereza imethibitisha kuwa wanajeshi watatu waliouwawa hapo jana katika shambulio la bomu walikuwa raia wa Uingereza.Wanajeshi tisa kutoka Afghanistan pia walifariki katika shambulio hilo la bomu ya kutegwa kando ya barabara.Vifo hivyo vya jana vimefikisha 444 idadi ya wanajeshi wa Uingereza waliouwawa Afghanistan tangu mwaka 2011.Mapema leo wanamgambo walimuua afisa mmoja wa baraza kuu la amani Malim Shawali pamoja na mlinzi wake katika jimbo la Helmand.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO