Kiongozi wa chama Kiislamu cha Enahdha nchini Tunisia Rashid al Ghanoushi amesema katiba mpya ya Tunisia imeandikwa kwa mujibu wa misingi ya Kiislamu. Akizungumza Jumamosi mjini Tunis katika semina iliyokuwa na anwani ya 'Kutekeleza Uislamu katika Siasa', Ghanushi alisema Baraza la Waasisi Tunisia lilitumia misingi ya Kiislamu kuandika katiba mpya ya nchi hiyo. Ghanushi ambaye ni mkuu wa chama cha Enahdha kinachoongoza muungano tawala nchini humo amesema katiba mpya imetegemea Uislamu kwa kuzingatia hali inayotawala ulimwengu wa sasa.
Mwezi ujao wa Juni Baraza la Waasisi Tunisia linatazamiwa kuchunguza rasimu ya katiba mpya ili hatimaye katiba hiyo iidhinishwe na wananchi katika kura ya maoni.
Tunisia ni kati ya nchi ambazo zimeshuhudia mwamko wa Kiislamu ambapo mtawala kibaraka wa nchi hiyo dikteta Zainul Abidin Bin Ali alitimuliwa madarakani 2011.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO