Kesi ya Hosni Mubarak, dikteta wa Misri aliyeng’olewa madarakani pamoja na wanawe wawili wa kiume Alaa na Jamal, waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani wa utawala wake Habib El-Adly pamoja na wasaidizi wake sita waandamizi imeanza kusikilizwa tena leo lakini imeakhirishwa hadi tarehe 8 Juni. Mubarak ambaye mwezi Juni mwaka jana alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kushindwa kuwalinda raia wasio na silaha katika vuguvugu la siku 18 la Mapinduzi ya wananchi yaliyoung’oa madarakani utawala wake wa kidikteta mapema Februari mwaka 2011 alifunguliwa tena mashtaka mwezi Januari mwaka huu kutokana na ukiukaji wa taratibu uliofanyika wakati aliposhtakiwa mara ya kwanza. Itakumbukwa kuwa Jaji Mustafa Hassan Abdullah aliyesikiliza kwanza kesi ya diktetka Mubarak na wenzake alijiondoa kusikiliza kesi hiyo mwezi uliopita na kuihamishia kwenye mahakama ya rufaa. Kesi hiyo sasa inasikilizwa na Jaji Mahmoud kamel El Rashidi ambaye ameaiahirisha hadi tareh 8 Juni ili kutoa fursa kwa mahakama ya kupitia nyaraka za ushahidi zenye kurasa 55,000…/
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO