Harakati ya Wananchi kwa Ajili ya Ukombozi wa Palestina – Kamandi Kuu (PFLP – GC) ambayo ina makao yake nchini Syria imetangaza kuwa inaunda vikosi vya wapiganaji kwa lengo la kuikomboa miinuko ya Golan ya Syria inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel. Uamuzi wa harakati hiyo umekuja baada ya Rais Bashar al – Assad wa Syria na harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah kutangaza kuwa wataunga mkono harakati yenye lengo la aina hiyo. Taarifa iliyotolewa na uongozi wa harakati hiyo ya mapambano ya Palestina imeeleza kuwa baada ya kimya cha karibu miaka 40 katika mpaka wa Syria na ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu iliyopewa jina la Israel harakati hiyo itaunda vikosi vya brigedi kwa lengo la kuzikomboa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel kwa kuanzia na Golan. Taarifa hiyo imeongeza kuwa harakati ya wananchi wa Palestina inafungua mlango kwa raia wote wa Syria kujitokeza katika kuunda harakati ya muqawama. Kufuatia mashambulio ya anga ya wiki iliyopita yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel ndani ya ardhi ya Syria, Rais Bashar al – Assad alisema ataigeuza Golan kuwa mstari wa mbele wa muqawama na kuruhusu wapiganaji wa muqawama kuishambulia Israel kutokea eneo hilo. Naye Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema harakati hiyo ya muqawama itasimama pamoja na harakati ya muqawama ya wananchi wa Syria na kuipatia uungaji mkono wa kimaada na kiroho kwa ajili ya kuikomboa miinuko ya Golan ya Syria
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO