Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania amewaaga askari 1,280 wa nchi hiyo wanaokwenda kujiunga na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa lengo la kupambana na makundi ya waasi.
Kikwete amewausia askari hao wakati akikabidhi bendera ya Tanzania kwa kikosi hicho kwamba, wajitahidi kulinda heshima na majukumu ya kazi zao. Askari hao wataunda kikosi kipya cha Umoja wa Mataifa kilichopangwa kuwa na askari 2,500, kilichoamuliwa kuundwa na Baraza la Usalama mwezi Machi, kwa lengo la kutekeleza operesheni za kijeshi dhidi ya makundi ya waasi mashariki mwa Kongo DRC.
Kundi la waasi wa M23 la Kongo lilitishia kuwaua wanajeshi wa Tanzania watakaojiunga na kikosi hicho.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO