Monday, May 06, 2013

MAKUNDI YA PALESTINA YATANGAZA KUWA TAYARI KUIJIBU ISRAEL

Makundi ya muqawama ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza yamesisitiza kuwa yako tayari kukabiliana na vitisho na mashambulizi yanayowezwa kuanzishwa na utawala haramu wa Kizayuni katika ukanda huo. Harakati za muqawama wa Kiislamu za Palestina yaani Hamas na Jihadul Islami leo zimetoa taarifa tofauti na kulaani mashambulizi ya ndege za kivita za utawala wa Kizayuni huko Syria. Hamas na Jihadul Islami zimesema kuwa zimejiandaa kikamilifu kukabiliana na mashambulizi yoyote ya kushtukiza ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza. Fauz Barhum msemaji wa harakati ya Hamas amesema kuwa mashambulizi ya Israel huko Syria ni ukiukaji hatari wa kujitawala na umoja wa ardhi ya nchi hiyo na kueleza kuwa kushindwa na kupata pigo mfululilizo Israel mbele ya muqawama wa Wapalestina kumeuchanganya utawala huo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO