Monday, May 06, 2013

RUSSIA YALAANI SHAMBULIZI LA ISRAEL LILILOUA WATU 42

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amelaani mashambulizi yaliyofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya kituo cha utafiti cha kijeshi nchini Syria na kusema kuwa, tukio hilo ni uchokozi wa wazi unaopaswa kulaaniwa na nchi zote duniani.
Alexander Lukashevich amesema Israel inajaribu kutia petroli kwenye moto unaoendelea kuwaka katika eneo la Mashariki ya Kati na akatahadharisha kuwa, moto huo ukisambaa zaidi utauchoma pia utawala huo ghasibu. Lukashevich amekumbusha kuwa ni kinyume cha sheria za kimataifa kuanzisha shambulizi dhidi ya nchi yoyote pasina sababu za kisheria.
Israel imedai mashambulizi hayo yalikuwa na lengo la kuizuia serikali ya Damascus kuipa silaha harakati ya Hizbullah ya Lebabon. Hata hivyo, Serikali ya Syria imekanusha tuhuma hizo na kusema Tel Aviv inajaribu kuishughulisha na shambulio hilo la kigaidi ili wapinzani wapate mwanya wa kujipenyeza zaidi.


Shirika la uangalizi wa haki za binaadamu nchini Syria, limesema kuwa mashambulizi ya angani ya Israel dhidi ya vituo vya kijeshi mjini Damascus, yaliua wanajeshi wa serikali wasiopungua 42. Mkurugenzi wa shirika hilo Rami Abdul-Rahman, ambaye ametoa idadi hiyo iliyorekebishwa leo, amesema kuwa wanajeshi wengine 100 ambao huwa katika vituo hivyo kwa kawida, hawajulikani walipo. Shirika hilo lenye makao yake jijini Londona Uingereza, awali lilisema wanajeshi wasiopungua 15 walikuwa wameuawa katika mashambulizi hayo ya mwishoni mwa wiki.
Syria inasema Israel ilivilenga vituo vitatu vya kijeshi karibu na mji mkuu Damascus mapema Jumapili, lakini haijatoa idadi rasmi ya waliokufa, ingawa wizara ya mambo ya kigeni ilisema katika barua iliyotumwa kwa Umoja wa mataifa, kuwa uvamizi wa Israel ulisababisha vifo, majeruhi na uharibifu mkubwa. Mashambulizi hayo yalikuwa ni ya pili katika kipindi cha wiki moja, ambapo Israel imevilenga vituo vya kijeshi vya Syria. Chanzo kutoa serikali ya israel kilisema mashambulizi hayo yalilenga kuharibu silaha zilizokuwa zinapelekwa kwa kundi la Hezbollah, la nchini Lebanon, ambalo linashirikiana na utawala wa rais Assad.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO