Sunday, May 05, 2013

MAMILIONI YA WAMALYSIA WAPIGA KURA

Mamilioni ya raia wa Malaysia wamepiga kura leo katika kinyang'anyiro kikali cha uchaguzi ambao huenda ukaiondoa madarakani serikali ya muungano ambayo imetawala kwa takriban miaka 56. Waziri Mkuu wa sasa Najib Razak ameelezea matumaini yake kuwa muungano wa National Front utabaki kuwa chama chenye nguvu zaidi kisiasa nchini Malaysia licha ya kukabiliwa na upinzani mkali tangu nchi hiyo ilipopata uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1957. Muungano wa vyama vitatu unaoongozwa na kiongozi wa Upinzani Anwar Ibrahim unatumai kuwa malalamiko ya umma kuhusu kiburi cha Muungano wa National Front, matumizi mabaya ya fedha za umma na ubaguzi wa rangi, yatawafanya wapiga kura kuuchagua upinzani kuingia madarakani. Tume ya Uchaguzi imesema kiasi ya watu milioni 8 wamepiga kura katika saa nne za kwanza za upigaji kura, ikiwa ni karibu aislimia 60 ya jumla ya wapiga kura waliosajiliwa milioni 13.3.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO