Sunday, May 05, 2013

MAHMOOD ABBAS AANZA ZIARA NCHINI CHINA

Rais wa Mamlaka ya ndani ya Palestina Mahmoud Abbas amewasili jijini Beijing, China, kwa ziara zasmi, huku Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pia akitarajiwa kukutana na maafisa wa China baadaye wiki hii. Shirika la habari la serikali Xinhua limesema Abbas atakuwa nchini China hadi Jumanne, wakati naye Netanyahu akitarajiwa kuwasili katika kitovu cha kiuchumi Shanghai kesho Jumatatu kwa ziara ya siku mbili kisha atazuru Beijing hadi Ijumaa. Abbas ameliambia shirika la habari la Xinhua kuwa anapanga kuwaeleza viongozi wa China kuhusu vizingiti vinavyokumba mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina na kuwaomba watumie uhusiano wao na Israel kuviondoa viziginti hivyo ambavyo vinaathiri uchumi wa Palestina. Naye Netanyahu anatarajiwa kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa China kuhusu kuwekewa vikwazo Iran katika jaribio la kusitisha mpango wake wa nyuklia, ambao Israel na nchi za magharibi zinashuku unalenga kutengeneza silaha za nyuklia.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO