Friday, May 10, 2013

UINGEREZA KUONDOA WANAJESHI WAKE LIBYA

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Uingereza, imewataka wafanyakazi wa ubalozi wake kuondoka nchini Libya, kwa kuhofia kukaririwa tukio lililoukumba ubalozi wa Marekani nchini humo. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kuzorota hali ya usalama nchini Libya. Uingereza imewataka wafanyakazi wa ubalozi wa nchi hiyo mjini Tripoli, kuondoka Libya mara moja. Hata hivyo Uingereza imeongeza katika ripoti yake hiyo kuwa, raia wake wataondoka Libya kwa kipindi kifupi tu hadi pale usalama utakaporejea. Hii ni katika hali ambayo, hivi karibuni Waziri wa Ulinzi nchini Libya Mohammed al-Barghathi alitangaza kubatilisha uamuzi wa kujiuzulu. Awali al-Barghathi alikuwa ametengaza nia yake ya kujiuzulu kama njia ya kulalamikia kitendo cha wanamgambo wenye silaha cha kuendelea kuzizingira baadhi ya wizara za nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO